Jifunze Kutotangaza Shida Zako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tatizo au shida humpata mwanadamu yeyote hapa duniani. Huo ndio ukweli wa maisha, kwani maisha ndivyo yalivyo. Kawaida, mtu akipata tatizo, hali yake hubadilika na tunaweza tukasema kuwa, mtu huyo huwa hayuko sawa. Anaweza akatafuta namna ya kutoka au kulitatua jambo linalomsibu. Kufanya hivyo ni hali ya kawaida sana.
Kuna matatizo ambayo mtu atahitaji msaada kutoka kwa watu wengine. Wakati mwingine, msaada unaweza kutafutwa kutoka sehemu fulani ambayo mtu anaona mwanga wa kusaidiwa. Msaada unaweza kuwa wa aina yoyote, aidha wa kimawazo ama ama wa kiuchumi.
Hebu tuangalie tatizo lipi linaweza kusaidiwa na nani au wapi. Yapo matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa kufanyiwa unasihi, lakini kuna yale ambayo yanaweza yakahitaji fedha. Inapofikia kuwa utatuzi unahitaji fedha, hapo inatakiwa uwe mwangalifu na makini zaidi. Eneo hilo la msaada wa kifedha linaweza kuwa lina udhalilishaji. Ni vema usitangaze shida zako. Wewe unaweza kuona una shida sana lakini kumbe unayemweleza, ana shida zaidi na kubwa kuliko zako.
Usipoangalia, huyo unayemweleza shida zako, anaweza akazitangaza kwa watu wengine. Ni vema ukajua unajianika kwa nani na anakuelewaje. Yakupasa ujionyeshe kuwa unaweza kujitegemea na siyo kujionyesha umeelemewa na matatizo yako. Kumbuka kupata na kukosa ndio maisha na humpata mwanadamu yeyote na hata huyo uliyemweleza huwa anapata na kukosa pia. Maisha ndivyo yalivyo.
Tunajifunza moyo wa kujitegemea na kujishugulisha katika maisha yetu. Kutangaza shida ama matatizo yetu, sana sana ni kujidhalilisha na kushusha hadhi zetu mbele za watu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection