Kuvunjika kwa Koleo, Sio Mwisho wa Uhunzi

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Uhunzi ni shughuli za ufundi chuma. Koleo ni chombo kinachotumika na mafundi wanaojishughulisha na masuala ya chuma. Endapo katika kukata chuma kikavunjika, kitakachofanyika ni kwenda kutafuta chuma kingine ili kazi iendelee.
Kwenye maisha yetu ya kawaida inawezekana na ni ukweli usiopingika pia kuwa unaweza kukwama katika kufanya jambo fulani. Pengine ni jambo ambalo ulikuwa unalitegemea sana. Endapo jambo hilo litashindikana, unaweza ukakata tamaa na pengine ukaamua kususa ama kuacha kabisa.
Mazungumzo haya yanatufundisha kuwa tusiwe tunakata tamaa kwenye jambo lolote. Umapokwama, badala ya kukata tamaa, anza upya na hatimaye utafanikisha.
Hata elimu tunaanzia chini. Hivyo, jambo lolote liwalo, lazima lianzie chini. Hali kadhalika, wafanya biashara wakubwa nao walianza chini. Ungepata fursa wakakueleza kule walikoanzia, unaweza usiamini. Lakini ukweli ni kwamba, ndivyo ilivyokuwa.
Tunashauriwa tuzingatie leo yetu ili tupate kwenda vile inavyotakiwa. Mathalani, leo kama biashara yako haikwenda vizuri, yakupasa uwe na mtizamo chanya ili kesho yako iwe nzuri. Siku hazifanani, yatupasa tujue hilo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection