Ni Rahisi Kubeba Kikombe Kisicho na Kitu Kuliko Kile Chenye Kitu

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwenye maisha ya binadamu, tunaposema “Ni rahisi kubeba kikombe kisicho na kitu kuliko kikombe chenye kitu“, ina maana kubwa. Kwa mfano, ukiishi na watu mbalimbali huku ukijivuna, ukiwadharau na kuwaona hawafai, hawajui kitu, ila wewe unajihesabia kuwa ndiye unayejua kila kitu, watu watakulinganisha au watakufananisha na kikombe kisicho na kitu chochote ndani yake, yaani kikombe kitupu.
Kwa kuwa utakuwa unaishi maisha yako yasiyoingiliana wala kujali mambo ya wenzio, ni wazi kuwa, watu wengi hawatakuheshimu bali watakudharau. Lakini kwa upande mwingine, ukiishi na watu vizuri kwa nidhamu, bila magomvi, bila dharau na kulinda heshima yako na ya watu wengine, watu watakuhesabu kuwa, wewe ni sawa na mtu aliyebeba kikombe chenye kitu ndani yake. Ina maana kuwa wewe ni mtu unayejali, mwenye heshima na mwenye utu kwa binadamu wenzio.
Tunafundishwa nini kwenye usemi huu?Funzo muhimu tunalopata ni kwamba yatupasa tuwajali na kuwaheshimu wenzetu. Hali kadhalika, tunatakiwa kushirikiana nao na kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wetu. Binadamu tunatakiwa kusaidiana pale inapobidi. Iwe ni mwiko kuwadharau wenzetu. Watu wenye dharau huwa na mwisho mbaya, na mara nyingi matokeo yake huwa ni fedheha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection