Mgeni Njoo, Mwenyeji Apone

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mgeni ni mtu anayekuja kwenye makazi ambayo hana mazoea nayo au ni mahali ambapo siyo kwake. Kwa kawaida, mtu huyu anapokuja humfanya mwenyeji wake kuhangaika kutafuta hiki na kile, ili mradi yeye na mgeni wake waweze kufurahi pamoja. Mgeni huyo anaweza kuwa ni ndugu ambaye ametoka mbali kuja kusalimia tu ama kwa shughuli nyingine. 

Mara nyingi, ujio wa mgeni hubadilisha kwa muda hali ya maisha na hata mpangilio wa chakula mle ndani. Kama ilipangwa kupika maharage basi itatafutwa mboga nyingine nzuri kama kuku au kitoweo chochote kile kizuri, tofauti na cha siku zingine. Suala la kubadili kwa muda utaratibu wa maisha huzingatiwa sana mgeni akija.

Wakati mwingine, hata kama kulikuwa na ugomvi au kutoelewana ndani ya nyumba, kuja kwa mgeni kunaweza kuwa ni suluhisho tosha kwa waliofarakana. Mgeni huyo huwa ni suluhisho bila hata kujua. Mara nyingi, watu wakigombana huita watu waje wawasuluhisha. Mgeni akija huweza kusawazisha hali hiyo na hivyo kufanya mtu mwingine wa nje asiombwe kuja kuwasuluhisha. Matokeo yake hubakia ni furaha na vicheko ndani ya nyumba pamoja na ratiba na aina ya chakula kubadilika hapo nyumbani.

Hii ndio maana kuu ya usemi huu wa ‘mgeni njoo, mwenyeji apone’. Nyumba inayopokea wageni mara nyingi hupata baraka, na wenyeji wake huneemeka kwa mambo mazuri yatakayotokea kutokana na ujio huo. Mambo mazuri kama chakula na vitu vingine huboreshwa kwa ajili ya mgeni. Furaha na amani huingia ndani ya nyumba hiyo iliyopata mgeni. Mifarakano, chuki na ugomvi huweza kwisha kutokana na ujio wa mgeni. Huko ndiko kupona kwenyewe.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Weka Bajeti Upate Mafanikio

Next
Next

Ni Rahisi Kubeba Kikombe Kisicho na Kitu Kuliko Kile Chenye Kitu