Weka Bajeti Upate Mafanikio

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna umuhimu wa kuwa na bajeti unapoanza au unapoendesha mradi wowote. Ili uweze kuidhibiti pesa ni lazima kuwa na bajeti. Ni muhimu kuwa na bajeti kwani itakusaidia kukuonesha pesa inatoka wapi na inakwenda wapi. 

Kuna msemo usemao, mali bila daftari, hupotea bila habari. Unapokuwa na bajeti katika mipango yako yote itakulazimu kuwa na nidhamu kwenye mapato na matumizi, ambayo mwisho wa siku ndio mafanikio katika shughuli zako. 

Mara nyingi ukiwa na bajeti itakusaidia kuwekeza mahali penye fursa nzuri, panapolipa vizuri zaidi na kwa wakati mwafaka. Ni vema kuwa bajeti kwenye miradi midogo na mikubwa ili uweze kurudisha mtaji na kupata faida kwa ajili ya uendelevu wa miradi. 

Kuwa na bajeti ni jambo la msingi sana kwenye maisha ya kila mwanadamu. Lazima tuzingatie hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Heshima Hutengenezwa kwa Hekima, Haitengenezwi kwa Mkiki

Next
Next

Mgeni Njoo, Mwenyeji Apone