Heshima Hutengenezwa kwa Hekima, Haitengenezwi kwa Mkiki

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mara nyingi tunapenda kumsifia mtu tunapoona kuwa ana heshima. Lakini hatuelewi kwa nini huyo mtu yuko vile alivyo. Silaha kubwa juu ya hilo ni hekima.
Hekima ni nguzo kubwa sana katika maisha. Ukiwa na hekima ni lazima utakuwa na heshima. Utamuheshimu kila mtu, awe mdogo ama mkubwa. Utakuwa kiongozi popote utakapokuwa. Kila mwenye tatizo atakuja kwako maana anaelewa hekima yako itamuongoza na kumtatulia shida au matatizo aliyokuwa nayo. Mara nyingi watu wenye hekima huwa ni wachache sana katika jamii.
Usemi huu unatufundisha kuwa hekima na kuheshimu binadamu wote bila kubagua rangi au imani ndio msingi wa maisha bora. Yatupasa tukumbuke kuwa sote ni viumbe wa Mungu na tumeumbwa kwa mfano wake. Kwa maana hiyo, heshima na hekima ndio viwe dira ya maisha yetu hapa duniani.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection