Maneno si Mkuki

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ulimi hutamka maneno yaani silabi zilizounganishwa zikaleta tamshi la kueleweka. Mkuki ni silaha ya jadi ambayo imetengenezwa kwa mti na ncha kali ya chuma. Mkuki hutumika kuwindia wanyama, hususani, wanyama wakubwa.
Tunaposema, maneno si mkuki tunamaanisha kuwa mwanadamu ana utashi. Asikiapo maneno yasiyopendeza masikioni mwake, kama vile maneno makali, maneno hasi, ya uchungu na yale ya kuchoma, anaweza kuyadharau. Kutokana na utashi alio nao, maneno hayo hayawezi kumchoma kama silaha yenye ncha kali.
Tunajifunza kuwa kama binadamu, tusikiapo maneno mabaya, maneno yanayochoma moyo na kuumiza, tunatakiwa tusiyazingatie ama kuyaweka moyoni, bali tuendelee na kazi zetu za kuleta maendeleo. Binadamu wengi ndivyo walivyo, kusema maneno makali ndio kazi yao. Lakini kama usemi usemi usemavyo, maneno si mkuki hivyo tusibabaishwe nayo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection