Udhaifu Wako Usikufanye Ujiwekee Ukuta Kuzuia Mafanikio

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Wakati mwingine binadamu tunakuwa na tabia ya kujidharau na kutojipenda. Huwa tunafikia hata hatua ya kujikataa na kujiona hatufai. Hali kadhalika, hujiona kuwa hatustahili kuishi na kwamba hata tukifanya kazi yoyote hatuwezi kupata mafanikio. Kuna wakati huwa tunakuwa na mtizamo hasi dhidi ya maisha yetu sisi wenyewe.

Inawezekana pia kuwa tumezaliwa na udhaifu wa kimaumbile. Pengine kuna wakati huwa tunawaza na kujiuliza kama jamii inaweza kutukubali na udhaifu tulio nao. Hata kama tumejaliwa kupata watoto, bado tunaweza kujiona kuwa kuna watu ambao wanatubeza, kutusimanga, na kutuambia kuwa maisha yetu yataishia kuwamabaya yasiyo na uhakika hadi mwisho wetu. Watu hao hujiona kuwa wana mamlaka ya kutuhukumu na kutuamulia hatima ya maisha yetu.

Hali ya mapito kama hayo au changamoto kama hizo zinaweza zikamvunja mtu moyo. Hali kadhalika, hali hiyo inaweza ikamfanya awe na mawazo mengi kiasi cha kujiona ni myonge, hana bahati,na akajihesabia makosa na hatima yake kukata tamaa ya kuishi.

Lakini katika maisha tunaambiwa kuwa, ‘Hujafa hujaumbika’. Tunatakiwa tujikaze, tujipe moyo kwani hao wanaotuwazia mabaya hawajatuumba wao. Hawana mamlaka na maisha yetu. Ieleweke kwamba, Mungu akiamua kukuheshimisha huwa haangalii mtu ana hali gani, ana nini, anafanya nini au yuko mahali gani. Ukweli ni kwamba, Mungu hutukirimia baraka zake kama alivyokukusudia. Hapa unalotakiwa kufanya ni kuikubali hali yako, muonekano wako na hata ulivyoumbwa. 

Kutokana na mazungumzo haya tunajifunza kuwa, si vema kujiwekea ukuta kutokana na udhaifu ulio nao au kutokana na makosa ya nyuma uliyowahi kuyafanya. Vilevile, inatupasa kujitahidi ili kuwa na mtizamo chanya kuhusu wewe mwenyewe kwenye maisha yako. Waswahili walinena, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Mambo yaliyopita yachukuliwe kuwa yamepita na hivyo inapasa kusonga mbele.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mpende Adui Yako

Next
Next

Maneno si Mkuki