Mpende Adui Yako

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Adui ni mtu ambaye  huna mahusiano mazuri naye. Mtu huyu utamtambua kuwa ni adui kwa matendo yake na hata kuongea kwake. Mara nyingi adui yako kila atakaloongea kwako huwa ni hasi na pia huwa halina amani. 

Hata hivyo, mtu wa namna hii hatakiwi kuonyeshwa ubaya. Pamoja na ubaya wake, anatakiwa kupendwa. Hata maandiko yanasema adui yako mpende. Katika hali ya kawaida huwa ni vigumu kuwa karibu na mtu kama huyu. Inatupasa tuwe na roho wa Mungu.

Kwenye simulizi hii, tunafundishwa kuwa si vema kulipiza kisasi kwa watu waliotufanyia ubaya. Pamoja na kwamba si rahisi sana kwetu sisi binadamu, bado tunatakiwa kuonyesha upendo. Hii ndio silaha kubwa sana katika maisha. Upendo huondoa tofauti kati ya mtu na mtu. Upendo hujenga amani na utulivu katika jamii zetu. 

Hali kadhalika, tunajifunza kuwa mwenye uvumilivu na upendo hushinda ubaya, badala yake wema hunatawala. Upendo ukitawala katikati yetu, Mungu atakuwa nasi na amani itakuwepo

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Nyakati Ngumu Ndio Thibitisho la Ujasiri Wako

Next
Next

Udhaifu Wako Usikufanye Ujiwekee Ukuta Kuzuia Mafanikio