Nyakati Ngumu Ndio Thibitisho la Ujasiri Wako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Nyakati ngumu ni kipindi ambacho kila mtu hupitia katika maisha yake. Katika kipindi hicho, inawezekana hali ya uchumi ikawa imeyumba na kuyafanya mambo yasiende ipasavyo. Kama una ujasiri, hali hiyo haitakuchanganya bali utaendelea kuwa na amani. Lakini usipokuwa jasiri, kila mtu ataelewa kuwa unapitia kwenye hali ngumu, hiyo haitakuwa sahihi hata kidogo.
Elewa kuwa hiyo hali haiwezi kuwa ya kudumu, ni ya muda tu. Na isitoshe, kila mtu hupitia hali kama hiyo, hauko peke yako. Ikumbukwe pia ipo siku lazima hali hiyo itapita. Maisha ndivyo yalivyo.
Usemi huu unatufundisha kutokukata tamaa kwa jambo lolote na kuwa makini katika maisha yetu ya kila siku. Tunapopatwa na misukosuko au mitikisiko ya maisha, yatupasa tuonyeshe ujasiri wa kuyakabili. Haijalishi ni matatizo ama mapito ya uzito wa kiasi gani, iwe ya uchumi ama ya maisha kwa ujumla, yatulazimu tuyakabili na kuyadhibiti. Hakuna lisilowezekana kama umedhamiria kuyashinda mapito kwa ujasiri
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection