Maji Yanayokimbia Huyapitia Maji Yaliyosimama

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Maji yanayokimbia mara nyingi ni maji ya kwenye mto. Na kuna yale maji yoliyotuama au kusimama yapo kando ambayo yawezekana yamekwamishwa na majani au kuzidiwa na udongo. 

Katika maisha pia kunakuwa na watu waliofanikiwa kimaisha na wengine hawajafanikiwa kabisa. Watu hawa kila kukicha huhangaika kujikwamua kutafuta mtaji au kazi ili watoke pale walipo. Lakini pamoja na jitihada hizo bado hawafanikiwi.  

Sasa wewe ambaye Mungu kakupa kazi na umejaliwa kipato kizuri, unapomuona binadamu mwenzio aliyekwama, yakupasa umsaidie ili na yeye aweze kutoka pale na kwenda mbele na wewe ili safari yenu iwe moja.

Huwezi kujua na wewe yatakayokupata huko mbele ya safari. Huenda nawe ukaja ukakwama halafu naye akaja kukusaidia. Maisha ni mzunguko. Maisha ni kitendawili kisichotenguliwa kiurahisi. Kumbuka, unapopata riziki, kula na wenzako uchoyo siyo jambo jema.

Simulizi hii inatufundisha mambo mengi ya msingi. Inatufundisha kuwa na utu, kuwa na uungwana na mioyo iliyosheheni upendo. Tunafundishwa tabia ya kujaliana na binadamu wenzetu. Tunakumbushwa uhalisia wa maisha, kwamba kuna kupata na kukosa, njia ambayo kila mtu hupitia. 

Ni afadhali kula pilipili ukasikia uchungu lakini mwisho ukasikia tamu, kuliko kula asali, mwisho wake ukasikia uchungu. Maisha ni kigeugeu, maisha hayana fomula maalum. Yatupasa tuyaishi vile yanavyotujia. Upendo uwe moja ya misingi na dira ya maisha yetu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mvuvi Ajua Pweza Alipo

Next
Next

Nyakati Ngumu Ndio Thibitisho la Ujasiri Wako