Mvuvi Ajua Pweza Alipo

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mvuvi ni mtu anayevua samaki kwa ajili ya biashara. Akifanikiwa kupata samaki wengi, wengine huwaacha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Hiyo ndio kawaida ya wavuvi. Pweza ni samaki anayependwa sana na watu hasa watu waisio ukanda wa pwani. Pweza huwa wanauzwa kwa bei mbaya sana.
Tunaposema "mvuvi ajua pweza alipo" tuna maana kuwa anayefanya kazi ya kuvua samaki lazima atajua samaki wakubwa walipo kutokana na uzoefu alio nao. Tunajifunza kuwa ukiwa mzoefu wa kilimo cha biashara kwa mfano, utajua vema zao lipi litaleta tija ama la.
Watu wengi tuna tabia ya kuiga mambo kutoka kwa watu. Ukiona mwenzio anafanya biashara hii na wewe unaiga biashara hiyo hiyo, mwisho wa siku kunakuwa hakuna wateja kwa sababu wenye bidhaa mko wengi.
Tunashauriwa tuache kuigana. Mathalani, kama ni kilimo, tutafute mazao mengine ambayo yataleta usitawi wako. Siyo wakulina wote muwe mnalima zao moja tu, mathalani, mahindi. Kwa mfano, inasemekana kuwa zao la vanilla huuzwa hadi kufikia milioni moja kwa kilo. Lakini wengi hatulitilii maanani. Tunasubiri kwanza tuone wangapi watalima zai hilo ili nasi tuige. Yatupasa tuwe na moyo wa ubunifu na uthubutu ili tuweze kujikwamua kiuchumi. Bila uthubutu katika maisha, binadamu hatuwezi kufika mbali. Riziki iko kila mahali, kazi kwako ewe mwanadamu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection