Ili Upokee Unahitaji Maandalizi

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Baadhi ya vitu kwenye maisha yako utachelewa kuvipata. Kuchelewa huko, haina maana kuwa Mungu hataki uvipate, bali ni kwa sababu Mungu anakupa muda wa kujiandaa kwanza.

Kila baraka mpya inayokuja kwenye maisha yako huwa inakuja na aina mpya ya vita. Yaani, ukipata cheo kipya basi jiandae kupambana na aina mpya ya vita ambayo haujawahi kuwa nayo maishani.

Ukiongeza mtaji kuna vita mpya itaibuka ya kiwango kingine kabisa. Watu wataanza kuona wivu na kujiuliza wao kwa wao kule ulikoutoa mtaji. Si hivyo tu, kipaji chako kikianza kusikika, wale watu ambao mlikuwa marafiki, wataanza kuwa maadui zako. Mwanadamu ni kiumbe mzito, haeleweki kabisa.

Ili kupambana na yote haya, unahitaji stamina mpya ili kuweza kuzikabili vita zinzokuijia kwa kasi. Stamina unayohitaji siyo ile ya kawaida, bali ya kiwango kingine kabisa.

Kuna baadhi ya watu, baada ya kupata baraka za kiwango cha juu zaidi ya walichonacho walikuta kuwa ndio unakuwa mwanzo wao wa kuharibikiwa.
Lakini tunachotakiwa kufanya, badala ya kulalamika tu, ni kuendelea kukabiliana na hiyo hali maana unakoelekea kuna dalili nzuri na ndiko kwenye furaha na amani. Tunachotakiwa ni kuwa na mtizamo chanya na ndipo tutakapoweza kufanikiwa zaidi na zaidi

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Uaminifu Ni Silaha Ya Mafanikio

Next
Next

Kila Mtu Ana Mfariji Wake