Uaminifu Ni Silaha Ya Mafanikio

Masimulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tunapozungumzia uaminifu tunakuwa na maana nyingi. Lakini maana kuu ni ile hali ya kuona kwamba cha mwenzio ni cha mwenzio, usiktamani. Cha msingi, ni kuridhika na cha kwako kwani hiyo ndio halali yako. Unapokosa kuwa mwaminifu kwa kile cha mwenzio ni kwamba unatafuta umaskini wa kujitakia.
Palitokea msichana mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi kwamama mmoja. Huyo mama alikuwa ana pesa. Mara nyingi alikuwa anaacha kiasi cha pesa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na vilevile alikuwa anaacha pesa chumbani kwake mezani ili kumpima yule binti maana alikuwa anaingia chumbani kufanya usafi. Alifanya hivyo mara nyingi lakini yule binti hakuwahi kuzichukua hata siku moja. Sana sana, alichofanya ni kumwambia mama akirudi jioni kuwa hela alizoziacha, amezitunza mahali fulani.
Yule mama, baada ya kufanya jaribio hilo kwa muda mrefu, aliamua kumueleza ukweli ya kwamba alikuwa anamfanyia kusudi ili aupime uaminifu wake. Haikuchukua muda yule binti akapata mchumba. Yule mwajiri wake aliwaambia wazazi wa huyo binti kuwa yeye ndiye atakayemfanyia sherehe.
Shughuli ilifanyika, wazazi walikuja kuhudhuria tu na kuchukua mahari ya binti yao. Hali kadhalika, alimpa zawadi ya kiwanja na kumfungulia biashara ya duka.
Wazazi walifurahi sana kwa ukarimu aliowafanyia. Binti aliishi vizuri na mume wake. Uaminifu wake ulimpa mafanikio bila ya kutegemea.
Kutokana na simulizi hii, tunaaswa kuwa waaminifu katika maisha yetu. Uaminifu ni silaha kubwa sana ya mafanikio. Aliyoyapata huyu binti aliyekuwa mwaminifu, ni ushuhuda tosha ya malipo ya uaminifu wake kwa yule mama aliyekuwa akimfanyia kazi. Tamaa hazijengi katika maisha, bali kuridhika na kile ulichonacho ni ufunguo wa mafaniko mengi ya mbeleni.
The Healing Hands Project
We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy