Heshima Haina Duka

Masimulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Heshima ni ile hali ya kumtambua mtu katika nafasi yake. Nafasi ya mtu hutokana na vile alivyoumbwa na mara nyingi mtu anazaliwa nayo. Kama anazaliwa nayo ni ya kwake, haiwezi kuwa ya mwingine.
Mara nyingi watu tunashindwa kuelewa kuwa huwezi kuchukua nafasi ya mtu mwingine, hata ufanyeje. Tunapoona fulani anafanya vizuri kwenye nafasi yake tunakuwa na ile hali ya kumuonea wivu na kumfanyia majungu ili atolewe pale, lakini kumbe ile ni nafasi yake. Wewe unayeitaka, hata ufanyeje, huwezi ukafanya sawasawa na yule, lazima kutakuwa na tofauti tu.
Heshima hutokana na neno hekima. Mwenye hekima lazima atakuwa na heshima na atafanya hivyo kwa kila mtu, iwe kwa mkubwa ama kwa mdogo. Hekima hutoka kwa Mungu. Ikumbukwe kuwa watu hamuwezi kulingana. Kila mtu aliumbwa kwa nyakati na majira yake.
Palitokea dada mmoja, aliyepewa nafasi ya kutumika sehemu fulani. Ukweli ni kwamba nafasi ile ilikuwa inamshinda, alikuwa haiwezi. Lakini kwa sababu alikuwa ana mtu juu yake ambaye alikuwa anamtetea na kumlinda, haikuwa shida, aliendelea kuishikilia nafasi hiyo pamoja na mapungufu hayo.
Ilifika wakati ikaonekana kuwa dada huyo nafasi hiyo haiwezi kabisa. Mbaya zaidi, nafasi hiyo ilikuwa ni ya mtu mwingine aliyeondolewa ili nafasi hiyo sipste dada huyu. Yule aliyeondolewa, kwa kweli alikuwa akiimudu sana ile nafasi. Hivyo kwa tahayari, ilibidi yule dada atolewe na arudishwe yule wa kwanza. Pamoja na kwamba ilikuwa ni vigumu sana kwa dada yule kukubali mabadiliko hayo, ilibidi iwe hivyo kwa sababu mambo yalikuwa yanaenda visivyo.
Usemi huu unatufundisha kuwa kila mtu ana cha kwake ambacho Muumba wake amempa. Ndiyo maana tunasema, heshima hainunuliwi na hai kadhalika, hekima hainunuliwi pia.
Sambamba na usemi huu kuna usemi usemao, ‘Usione Vyaelea, Vimeundwa’. Cha msingi ni kuwa kila mtu yampasa aombe kuwa na hekima ili aweze kuishi vizuri na jamii inayomzunguka. Bila hekima, maisha ya mwanadamu huwa siyo mazuri, bali huwa ni ya kubahatisha.
The Healing Hands Project
We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy