Rafiki Wa Kwali Ni Yule Anayefahamu Matatizo Yako Na Bado Uko Naye

Masimulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Hapa duniani tuna makundi mengi ambayo tunaishi nayo siku hadi siku. Makundi hayo yamegawanyika kutokana na hali halisi ya maisha. Kuna kundi la familia, ndugu, marafiki, na pia wale unaofanya nao kazi. Kundi hili la mwisho, kazi ndio inakuwa kiunganishi kikubwa..
Kundi la marafiki huwa ni kubwa zaidi. Kundi hilo linaweza kuwa ni zuri au la kinafiki . Kuna rafiki ambaye anakuwa ni kama ndugu unaweza usimtofautishe na ndugu wa familia yako. Rafiki unaweza ukamuamini kiasi kwamba kila jambo lako utamshirikisha, liwe baya au zuri.
Katika marafiki inabidi uangalie yule ambaye anaweza kubeba siri zako na kwamba kama umemshirikirsha, basi usije ukazisikia sehemu yoyote. Hapo unahitaji umakini wa kufahamu mtu aliye sahihi. Ukikosea basi utaangukia pabaya.
Umakini wako utakupa rafiki mzuri na wa kweli. Rafiki huyo huwa yuko tayari kubeba matatizo yako pindi yanapotokea. Mwingine anaweza akakuacha njia panda ukihangaika peke yako. Rafiki wa aina hiyo sio rafiki mzuri .
Rafiki mzuri na wa kweli, ni yule anayekufaa wakati wa shida. Ni yule anayeona tatizo lako kama la kwake the na anakuwa tayari kukutetea kwa hali na mali, kwenye jambo dogo ama kubwa, kuwe na mvua ama jua, yeye anakuwa mstari wa mbele kukusaidia wakati wowote na kwa hali yoyote, ili mradi wewe upate msaada unaouhitaji kwa wakati muafaka. Marafiki wa namna hii kwa hakika si wengi, ni wachache mno. Ukiwa nao, yakupasa umshukuru Mungu, na uwasike vizuri, usiwaachilie.
The Healing Hands Project
We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy