Ni Rahisi Kusikia Maneno ya Mdomoni Kuliko Ya Moyoni

Masimulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kilichopo ndani ya moyo wa mtu ni vigumu sana kukijua hata kama ni ndugu yako au rafiki yako. Waswahili walisema, moyo wa mtu ni msitu mnene ambao unatoa maamuzi yaliyo sahihi au magumu. Yawezekana kabisa jambo ambalo litaamuliwa na moyo likakinzana na fikra ya mtu lakini kwa sababu moyo hauna mshauri basi maamuzi yanaweza kuwa ni mabaya. Ubaya wake utaonekana baadae wakati ambao inakuwa vigumu kubadilisha.
Ni rahisi kusikia yatokayo mdomoni mwa binadamu. Yale tatokayo mdomoni yanaweza kurekebishwa. Yaliyo moyoni, huwezi ukafanya chochote.
Sambamba na hilo, kuna usemi usemao, ‘kuna kitu usichokijua nyuma ya tabasamu ya mtu’. Usemi huu una maana kuwa mtu anaweza akaonyesha tabasamu mbele yako, kumbe moyo wake unavuja damu na ana huzuni kwa iliyosababishwa na wewe kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kwa vile wewe huoni kilicho moyoni mwake unafikiri mambo yako sawa, unaongea naye vizuri tu naye haonyeshi chuki yoyote.
Ukweli ni kwamba, huwezi kukiona kilicho ndani ya moyo wa mtu kwa kuangalia na macho. Hebu jaribu kuiangalia jamii au marafiki ambao unaishi nao kila siku, jifunze kutoka kwao na jaribu kuwaelewa.
Binadamu ni kiumbe mzito sana. Kumuelewa ni kazi kubwa. Moyo wake huficha mengi kuliko yale tunayoyasikia kutoka kwenye midomo ya watu. Yatupasa tuwe makini.
The Healing Hands Project
We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy