Anayevumilia Mpaka Mwisho Ndiye Anayekula Akashiba

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuna jambo la kukatisha tamaa linaweza kutokea wakati imejikita na shughuli fulani halafu ukashindwa kuvumilia na pengine hata ukatangaza kuwa umechoka na wala hautaki tena kuendelea nalo. Hali hiyo ya kukata tamaa itakupelekea wewe kuacha unachofanya. Hatua hiyo siyo nzuri. Mvumilivu hula mbovu, wahenga walinena.
Ukianza biashara na ikafika mahali ukasema umechoshwa kwa vile biashara yako haiendi vizuri, hutaweza kuona mafanikio tarajiwa na utaiua hiyo biashara.na ikawa ndio mwisho wake.
Katika maisha yako hutakiwi kuchoka kwa jambo lolote unalolifanya. Wahenga walinena, ‘polepole ndio mwendo’. Ukiona unachoka badilisha mtazamo na hisia zako ziwe chanya. Maana ya usemi huo wa anayevumilia mpaka mwisho ndiye anayeshiba na kufanikiwa, una maana kubwa sana.
Unapopita katika majaribu na maumivu makali elewa kuwa unaelekea kushinda. Maumivu na majaribu hayo ni njia ya kukujenga na kukuimarisha. Acha kukata tamaa, vumilia hadi mwisho. Kumbuka, yupo yule aliyekuumba ambaye hutoa baraka zake kwako na kukuwezesha ili ustahimili na uweze kuvuka. Majaribu ni mtaji, waswahili walisema. Epuka kusema umechoka ili mema yaweze kukuijia kwa nguvu zote
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection