Ukitaka Salama Ya Dunia, Zuia Ulimi Wako

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili wa binadamu lakini kimebeba mambo makubwa na mazito. Kiungo hiki kimebeba magomvi, matusi, uchochezi, utenganishi na mambo mengine mengi ambayo yanaleta vurugu katika maisha ya jamii siku hadi siku.

Usemi huu unatuasa tudhibiti ndimi zetu. Endapo tunataka hali iwe ya utulivu na amani katika maisha yetu, inatupasa tuzuie ndimi zetu zisinene kila liwalo. Ulimi wako mara zote unapaswa unene maneno ya busara na hekima. Ukweli unaonyesha kuwa maneno mengi huwa yana maudhi kwa wengine wanaokusikiliza. Pale itakapotokea maneno ya maudhi yamesemwa mbele za watu, vurugu na mambo mengi huweza tokea kwenye familia au jamii zetu

Tunaaswa umuhimu wa kutumia ndimi zetu vizuri ili tuwe watu wa kuunganisha watu na watu wengine, na sio kuwatenganisha ama kubomoa mahusiano yaliyopo. Hali kadhalika, itatusaidia kuwa salama kwenye familia, jamii na watu wanaotuzunguka.

Usemi huu unatufundisha kuwa waangalifu kwa kila kinachotutoka vinywani mwetu maana ulimi ni wa hatari sana usipodhibitiwa. Ulimi unachonganisha. Ulimi unaua. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Subira Yavuta Kheri

Next
Next

Anayevumilia Mpaka Mwisho Ndiye Anayekula Akashiba