Kila Mtu Ana Mfariji Wake

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwenye kila majira ya maisha yako, kuna mtu anakuwa ameandaliwa kuwa mfariji wako. Mtu huyu anakuwa amepewa moyo wa kukuonea huruma ya kipekee na huwa yuko tayari kutumia muda wake kukufariji.
Mara nyingi sana watu wa namna hii wanaweza kuonekana kuwa ni wa kawaida sana na pengine hawana cheo, pesa wala mali. Kwa kifupi, hawa watu huwa ni watu wa kawaida kabisa.
Unachotakiwa kujua ni kuwa, watu wa namna hii, huwa hawajaletwa kukupa vitu, ila wameletwa kukupa faraja ambayo wenye mali, pesa na cheo hawawezi kukupatia.
Watu hawa wanaweza wasiwe na wewe kila siku. Inawezekana sio watu ambao unawapa kipaumbele. Lakini watu hawa ni wa pekee sana kwako. Wamepewa nguvu fulani ya kukuvusha kwenye magumu yako.
Hawa ni wale ambao ukiongea nao, ukitumia muda nao au ukiwaona au kuwasikiliza huwa unajihisi kama kuna mzigo mkubwa umeondolewa moyoni mwako.
Changamoto ya watu tulio wengi, watu hawa huwa tunawasahau kabisa pale wakishatusaidia. Hali kadhalika, huwa hatuwapi nafasi tena.
Tunashauriwa kuwa tusikimbilie kutafuta msaada kwa watu wenye pesa, mali na vyeo tu. Kila mtu anahitaji mtu wa kumfariji ili akusaidie pale unapohitaji.
Angalizo, kama ulishakuwa naye mtu wa namna hii na huna mawasiliano naye kwa sasa, mkumbuke leo, mtafute na umshukuru tena ili muweze kuendelea mahusiano yenu kama zamani. Unamhitaji.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection