Zawadi Haina Udogo

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Zawadi ni kitu chochote akupacho mtu bure bila kukiomba. Mtu anapokupa zawadi iwe ndogo au kubwa, unatakiwa kushukuru. Kutoa shukurani kwa vitu ama zawadi tunazopewa ni jambo la uungwana kwa mwanadamu yeyote.
Kuna watu wengine huweza kunung'unika wanapopewa zawadi, hasa pale zawadi inapokuwa ndogo. Lakini ni busara kukumbuka kuwa zawadi aliyopewa hakuitegemea, bali mtoaji alijisikia tu kumpa. Angeweza hata asimpe kabisa. Ni hiari ya mtoaji.
Ndio maana tunasema kuwa, zawadi ni zawadi, haina udogo wala ukubwa. Kutokana na ukweli huo, kama mpokeaji, inakupasa kuridhika, kuifurahia na kumshukuru yule aliyekupatia.
Funzo kubwa tunalolipata hapa ni kuwa na shukurani pale tunapopewa zawadi. Yatupasa turidhike na kushukuru kwa sababu hicho ulichopewa, hakikuwa haki yako. Kutokushukuru kwa vitu vidogo tunavyopata ni dalili kuwa hata tukipata vikubwa hatutaweza kushukuru. Kila mwanadamu anapaswa kujenga tabia ya kushukuru. Neno ahsante, hufungua milango mingi ya kupokea.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection