Mjinga Mpe Nafasi

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tukiangalia tafsiri ya mtu mjinga tunaona kama vile ni mtu asiyefaa kwenye jamii au ndani ya familia. Mtu kama huyo hudharaulika sana hata kama akisema au akiongea kitu huwa anapuuzwa, wala hatiliwi maanani.
Msemo huu una maana kubwa sana kwa kuwa unatambua na kuthamini nafasi ya kila mtu katika jamii.
Huyo mtu anayeitwa na kuonekana kuwa ni mjinga, ana mchango mkubwa sana katika jamii au ndani ya familia. Watu wa aina hiyo wakipewa nafasi ya kuongea huwa wanasema hovyo hovyo, ama husema chochote. Lakini hiyo hovyo yao hugeuka kuwa yenye maana nzuri kwenye mada husika.
Kwa ujumla maneno mengi ya mtu mjinga huchangia katika kurekebisha mambo mengi kwenye jamii au familia kwa sababu yeye huwa haoni aibu kusema chochote, mahali popote lile jambo linalomkera. Akiwa kwenye mikutano ya hadhara, yeye huwa anamwaga sera iwe mbivu au mbichi. Yeye anachokitaka ni kwamba ujumbe ufike kwa mhusika/wahusika.
Kutokana na msemo huo, tunajifunza kuwa tusiwadharau wale tunaowaona kuwa ni wajinga. Hata wao wana sehemu yao katika jamii au ndani ya familia. Kuna vitu vingine vinahitaji watu kama hao, watu wanaoweza kuongea ukweli bila kujali wala kuogopa. Hata mbele ya viongozi wetu wa kiserikali au wa kimila, hao ndiyo huwa wanaibua mambo bila woga. Viongozi nao wanapopashwa ukweli na watu ambao huonekana ni wajinga, huguswa na hivyo huweza kutekeleza kwa kuwa ukweli wa jambo umewekwa wazi.
Katika hali ya kawaida, watu kama hao hawawezi kulinyamazia jambo lonalowakera. Uwazi na ukweli wa watu hawa huchangia maendeleo ya mahala husika. Mara nyingi, uwazi wao huwakumbusha wahusika wajibu wao katika jamii. Kwa maana hiyo, kila mtu ana mchango wa kutoa katika jamii anayoishi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection