Uwe Mkweli Na Mwenye Maamuzi Sahihi

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuna mambo ambayo unatakiwa kuzingatia katika maisha yako. Mojawapo ya mambo haya ni kufanya maamuzi sahihi. Ukweli unaonyesha kuwa maskini walio wengi na watu ambao wameshindwa kuendesha biashara ama waliokwama kwenda mbele, ni wale ambao wana tabia ya kushikilia mambo ya jana. Ukweli ni kwamba, jana ilikwishapita na hivyo haiwezi kukupa chochote.
Kumbuka, usifanye vitu kama ulivyokuwa unafanya jana. Jifunze kufanya vitu vipya kila siku. Kuwa mbunifu maana kila siku kuna mambo mpya ya kujifunza. Pale utakaposahau ya jana, utaweza kupata kesho yako. Maisha ndivyo yalivyo.
Unachohitaji ni kufanya maamuzi sahihi kwa kusahau yaliyopita na kuangalia kesho yako. Kuwa mkweli na mwenye msimamo thabiti ili uweze kuyashinda haya maisha yenye kupanda na kushuka.
Mafanikio yatakuja endapo utakuwa mkweli na mwenye msimamo imara. Yaliyopita yasikuumize wala yasikufanye ujione kuwa huna thamani au ujione umeaibika. Cha msingi, unatakiwa kufanya maamuzi sahihi na Mungu atakubariki na kukunyooshea mapito yako.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection