Unaweza Ukawa Mkwezi Na Usiweze Kusuka Pakacha

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mkwezi ni mtu ambaye huwa anaangua nazi. Pakacha ni kifaa kinachosukwa kwa kutumia makuti ya minazi ili kubebea nazi na hata vitu vingine.
Kutokana na usemi huu, tunafundishwa kuwa Mwenyezi Mungu ametuumba ili tuwe tunategemeana. Kila mtu analo jambo ambalo amejaliwa kulijua, tofauti na mwingine. Hii ndio maana na sababu ya kutegemeana. Kila mtu anamtegemea mwingine, hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna mambo mengine ambayo huwezi kuyafanya ukiwa peke yako.
Usemi huu ni uthibitisho tosha wa kutegemeana kwa binadamu. Kazi ya mkwezi ni kuangua nazi na mtu mwingine atasuka pakacha na mambo yanaendelea bila wasiwasi.
Kwa maana hii, tunaaswa kutokumdharau mtu yeyote katika nafasi aliyokuwa nayo. Ipo siku utamhitaji mtu mwingine, awe mdogo ama mkubwa, yote ni sawa, kwa ajili ya kukamilisha malengo yako. Sambamba na ukweli huo, heshima ni kitu cha bure, mtu hahitaji kwenda shule kujifunza. Kila mtu ana nafasi na umuhimu katika jamii anayoishi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection