Hasara Haiogopi Mtaji

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mtaji ni nyenzo ambayo inatumika kwa ajili ya kutengeneza jambo fulani lenye tija ndani yake. Inawezekana ikawa ni fedha au kitu kingine ili mradi kiweze kuleta tija. Mtaji unatakiwa uzalishe na utoe faida. Ili iweze kuwa hivyo, unahitajika umakini wa hali ya juu endapo utataka kufikia malengo uliyojipangia.
Umakini unatakiwa katika matumizi unayofanya wakati unaendelea na mchakato huo. Kwa mfano, huwezi kutumia mtaji wa biashara nje ya biashara iliyodhamiriwa. Unapochanganya biashara mbili kwa mtaji moja, jua kabisa unatafuta hasara.
Haijalishi ukubwa wa mtaji, kama hutakuwa makini, utakuwa unakaribisha hasara. Hasara haiangalii ukubwa wa mtaji, bali inaangalia umakini wa kuutendea kazi.
Kuna watu wengine wakipata fedha huwa wanabadili mfumo wao wa maisha. Matumizi yao ya kila siku hubadilika. Hupenda kuiga maisha ya kifahari ambayo siyo stahiki yao. Hali kadhalika, husahau walikotoka. Kwa kuiga iga bila mpangilio, hasara huja kiulaini bila vikwazo vyovyote.
Usemi huu unatufundisha kuwa makini katika matumizi yetu kwa sababu, hasara haiogopi mtaji ulionao. Tusipende kuiga mambo ya wenzetu na kujifanya matawi ya juu, wakati kiuhalisia, wewe ni mtu wa kawaida, wa hali ya chini. Yatupasa tuwe waangalifu na matumizi yetu ya fedha. Kuwa na malengo thabiti ni muhimu katika maisha ya mwanadamu yeyote. Tumia mtaji wako vizuri ili uweze kukuletea maendeleo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection