Kikulacho Ki Nguoni Mwako

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Siyo watu wote hapa duniani ni marafiki wazuri. Wapo marafiki wengine ambao ni wabaya, wanafiki, wambeya, wakweli, waongo, na kadhalika.

Mara nying, mtu anayekufanyia ubaya huwa ni rafiki yako wa karibu sana ambaye katika hali ya kawaida, hutegemei akufanyie ubaya. Wewe unaweza kuwa unamwamini sana kutokana na ukaribu mliokuwa nao. Na unaweza kuwa unammegea siri zako za ndani wakati mwenzio yuko nawe kwa ajili ya kukuchora na kuyachota yako ya moyoni ilibaweze kuyatangaza kwa watu kwa faida aijuaye yeye.
Binadamu kiumbe hatari sana

Kwa upande mwingine rafiki wa kweli ni yule anayekujali kwa kila hali, anayeshirikiana nawe vizuri katika shida na raha. Marafiki kama hao siyo wengi sana, lakini wapo. Ukibahatika kuwa nao, thamini fursa hiyo, ni hazina kubwa. Yakupasa uitunze sana tunu hiyo.

Kuna usemi wa ‘Kikulacho ki nguoni mwako’, usemi ambao hutumika mara nyingi sana. Ni usemi wenye maana kubwa sana. Kumbuka, mtu anayekufanyia jambo baya, mara nyingi huwa ni rafiki yako wa karibu ambaye hatoki mbali. Rafiki huyu huwa anayajua mambo yako yote na hata yale ya ndani. Akiyaanika mambo yako kila mtu anaweza kuamini kutokana na ukaribu mlio kuwa nao.

Vilevile, msemo mwingine unaofanana na huo na wenye tafsiri sawa ni ule usemao, ‘Maji yanayozamisha meli siyo yale ya nje bali ni yale yaliyoingia ndani yake’. Msemo huu unathibitisha zaidi ukweli ule usemao, kikulacho kiko ndani yako mwenyewe.

Kutokana na simulizi hii tunajifunza umuhimu wa kupembue marafiki zetu ili tuweze kujua yupi ni rafiki wa kweli ambaye utaweza kumuingiza moyoni mwako. Hivyo tuwe makini sana kwani siyo kila rafiki ni rafiki mzuri au wa kweli.
Yatupasa tuwe waangalifu sana na maisha yetu yanayohusisha marafiki.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hasara Haiogopi Mtaji

Next
Next

Muongo Huwa Haulizwi