Muongo Huwa Haulizwi

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Hapa duniani kuna watu wa aina mbalimbali. Ndio maana watu husema dunia ni uwanja wa fujo. Kuna makundi mengi yenye huluka tofauti tofauti. Katika makundi hayo liko kundi moja ambalo ni gumu sana nalo ni lile kundi la waongo au wazushi. Kazi kubwa ya kundi hili huwa ni kuvuruga jamii. Watu walioko kwenye kundi hili ni wa hatari sana. Wao ni mabingwa sana wa kuleta uchonganishi na kugonganisha watu ili wasielewane. Pale wanapoona fulani na fulani wanaelewana, wao hukosa raha. Lazima watatafuta njia ama namna ya kuwavuruga. Watajitahidi kutunga uongo unaoendana na ukweli ili mradi tu waweze kuwatenganisha.

Binadamu wengine ni hatari kweli kweli. Raha yao kubwa ni kuwaona marafiki wakivurugana na kugombana. Machafuko yanapotokea kwa hao wapendanao, wavuruga mahusiano hukaa pembeni na kuchekelea. Azma yao inakuwa imekamilika, na mioyo yao inakuwa imeridhika.

Watu hao huwa hawaulizwi na wala huwa hawaishiwi maneno ya kusema. Kila wanaemkuta, haijalishi wanamjua, wamemzoea au la, lazima watakuwa na la kusema kuhusu mtu mwingine. Hiyo ndio tabia yao, hiyo ndio huluka yao. Na ndio maana ya usemi huu wa ‘Mwongo huwa haulizwi’. Yeye hujiropokea chochote kuhusu mtu mwingine na wakati wowote. Watu wa namna hii ni wa kuepukwa sana. Yatupasa tuwe mbali nao.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kikulacho Ki Nguoni Mwako

Next
Next

Kunguru Hashibi Jalala Moja