Kunguru Hashibi Jalala Moja

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

KUNGURU HASHIBI JALALA MOJA

Maisha ni kukimbizana kwa kila hali. Katika jitihada za kutafuta huku, kinachotakiwa ni kujaribu hiki na kile bila ya kuchagua nini cha kufanya. Hii ina maana kuwa, kila unachokifanya kitakuwa na matokeo yake.

Tunatakiwa kufanya kila kitu ambacho kitaleta tija. Cha msingi, itatubidi tuangalie nyakati na majira ya kufanya jambo husika.

Usemi huu unatufundisha kutokuchagua kazi. Waswahili husema, ‘kazi ni kazi ili mradi mkono uende kinywani’. Upatapo mpenyo wa kufanya biashara fulani fanya lakini uangalie, isije ikakuchanganya na hatimaye, ukaja kuambulia hasara. Kama kunguru alivyo, yeye hakai kwenye jalala moja. Huruka hapa na pale ili kutafuta riziki sehemu nyingine na pia ili aweze kupata vitu vingine tofauti na vile anavyopata kila siku

Kama binadamu, hatutakiwi kuchagua kazi, bali tunatakiwa kufanya kile kinachokuja mbele yetu. Yatupasa tuzingatie ukweli kuwa kupata na kukosa ndio mwendo. Vijana wanaaswa kutoangalia elimu waliyokuwa nayo, isiwafanye wawe wanachagua kazi. Inawapasa waangalie maisha ya kesho. Kila kazi huwa inalipa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Muongo Huwa Haulizwi

Next
Next

Hata Kobe Anafika Anakokwenda