Hata Kobe Anafika Anakokwenda

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Safari ni tendo la kutoka mahali na kuelekea mahali pengine. Inawezekana ni safari ya matembezi tu au inaweza kuwa ya kumtembelea ndugu au jamaa. Safari vilevile inaweza ikawa ni ya elimu kuelekea mafanikio. Hata kufanya biashara ni safari maana lazima uanze kidogo kidogo ndipo uweze kufikia malengo.
Usemi huu unatufundisha kuwa kila jambo lazima lianzie chini. Haijalishi unaanzaje, lakini watu husema, polepole ndio mwendo. Pia kuna msemo unaotuasa, ambao ni ‘Mwenda pole hajikwai’.
Katika maisha, tunaaswa kuwa chochote tunachofanya, yatupasa tufanye kwa malengo. Hali kadhalika, tufanye kwa kuzingatia muda. Kamwe usiangalie mwanadamu aliye mbele yako na kuanza kukata tamaa, kwani hata yeye kuna mahali alianzia. Na wewe pia utafika pale ulipokusudia. Haijalishi unatembea taratibu au vipi. Kuwa na imani kuwa utafika na kwamba ipo siku utafanikiwa. Mungu wetu ni mwema.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection