Mwamba Ngoma, Ngozi Huvutia Kwake

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Tunazungumza kuhusu upendo kati ya mtu na mtu na ndio Muumba wetu alivyotuagiza. Mara nyingi maisha yetu yametawaliwa na ubinafsi na uchoyo. Maana hakuna mtu atakuwa na mpenyo akamkumbuka mtu wa mbali kwanza kabla ya yule wa karibu naye. Zaidi ataanza na jamaa zake wa karibu kwanza.

Tunashuhudia hata katika teuzi mbalimbali zinazofanyika. Watu wanaoangaliwa na kupewa kipaumbele kwanza, ni wale ambao walifanya kazi pamoja au walisoma wote ama ni ndugu au jamaa wa karibu. Ukweli ni kwamba, huwezi kupika chakula ukampelekea jirani kabla watoto wako hawajala. Huu ni ubinadamu kabisa. Ndio maana ya mwamba ngoma huvutia ngozi kwake.

Mfano mwingine ni kama ule wa sisi wanasihi. Tulipooombwa tuongeze akina mama wengine kwa ajili ya kuingia kwenye zoezi la unasihi, kila mmoja wetu alimleta rafiki yake anayefahamiana naye vizuri. Huko nako tunaweza kusema, ni kuwamba ngoma kuvutia kwako. Tuliweza kuwaleta watu ambao tuna uhakika kuwa watafanya kazi vizuri bila kutuaibisha.

Kutokana na usemi huu, tunatukumbushwa kuwajali watu wetu wa karibu, watu wa nyumbani kwetu kwanza. Kumbuka, wahenga walinena, “Ibada njema huanzia nyumbani kabla ya kuingia sinagogi”, huo ndio ukweli wa maisha. Tunaaswa mambo mengi tu kwenye simulizi hii. Moja ya mafunzo ni kwamba, hatutakiwi kutengeneza kwa wenzetu kwanza wakati kwako kunabomoka. Kuna ukweli

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hata Kobe Anafika Anakokwenda

Next
Next

Mazoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita