Umdhaniaye Siye

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha, wengi wetu tunaangalia sana matendo ya mwanadamu kwa juu juu, bila kutafakari kwa undani mazingira halisi au asili ya mtu huyo. Mara nyingi jambo hili linajitokeza kwa watu ambao wameishi na kuaminiana kwa vile kila jambo linaenda vizuri na pia hapajawahi kutokea kasoro yoyote kati yao. 

Lakini kimsingi hakuna ambaye ni mkamilifu au asiye na mapungufu. Shida inakuja pale inapotokea mmoja wao atakapokwenda kinyume na taratibu zao, kwa sababu kila mmoja anamwamini sana mwenzake, hategemei kuwa kunaweza kukatokea kinyume chochote.

Mnapoishi wawili kuna wakati huwezi dhania kuwa mwenzio kuna jambo atakalofanya kwa yale mazoea mliyonayo. Lakini kwa uzoefu, haya ni ya kawaida kabisa katika maisha yetu. Mwenzio anaweza kufanya kitu mpaka ukajiuliza, hivi ni kweli au naota au nafananisha?

Tunachojifunza ni kwamba tuishi, tushirikiane na watu lakini usiweke dhana ya kuona kuwa mtu huyu hawezi kabisa akakufanyia jambo fulani baya au kunigeuka. Yatupasa tukumbuke kuwa umdhaniaye siye.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Usisamehe Kama Hauko Tayari Kusahau

Next
Next

Epuka Wasengenyaji