Epuka Wasengenyaji

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wasengenyaji ni watu wasiokuwa na kazi na huwa wanawasema wenzao bila sababu ya msingi. Watu hawa ni wa hatari sana kwani huwa wanatumia muda wao mwingi katika kujadili maisha ya watu wengine. Tunashauriwa kujiepushe kujenga urafiki na watu kama hao.
Watu wa aina hii, wakati ukiwa nao, watawajadili watu wengine. Itakapotokea ukawa mbali nao tu, wewe ndiye utageuka kuwa mjadala wao. Hawaaminiki. Hawatabiriki.
Hapa tunashauriwa kuwa tunapaswa kuchagua vizuri marafiki tunaotaka kuwa nao. Cha msingi ni kwamba yatupasa kujenga urafiki na watu ambao wanazungumza mambo ya maana na siyo mambo ya watu. Urafiki wetu uwe na wale watu wanaojitambua. Tunahitaji kuwa na watu wanaothamini utu wao, watu wanaojua sababu za kuishi kwao hapa duniani na si vinginevyo. Hatuhitaji kuwa na urafiki na watu ambao wapo wapo tu na mambo yao hayajulikani.
Kwa hiyo katika maisha yetu yatupasa , tujiepushe na watu wa namna hii kwani ni watu wa hatari sana.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection