Fimbo ya Mbali Haiui Nyoka

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wanadamu tumeumbwa kusaidiana. Usemi huu unatufundisha umuhimu wa kuishi vizuri na jamii inayotuzunguka. Hii ina maana kuwa ukipatwa na janga lolote, jirani yako ndiye atakuwa wa kwanza kuja kukusaidia na kukufariji. Haijalishi ni ndugu ama laa.
Wakati ndugu zako watakapofika kushughulikia tatizo lako, jirani zako wanakuwa tayari wameishafanya sehemu kubwa ya usaidizi kwako. Sambamba na usemi huu ni ule usemao ‘Halahala jirani’ au ‘Mbiu huanzia nyumbani’.
Hebu tuangalie jinsi TEWWY inavyodhihirisha usemi huu. Wanasihi wa TEWWY wengi ni watu ambao walijuana kabla ya kuanza kazi ya unasihi. Mnasihi wa kwanza aliwaleta akina mama ambao walikuwa wanafanya kazi Wizara moja. Ilikuwa rahisi kwake kuwaunganisha wenzie anaowajua tewwy kuliko kuwaleta wale asiowajua. Hapo ndio inathibitisha kuwa fimbo ya mbali haiui nyoka.
Tunaendelea kujifunza kuwa inatupasa tuwe na mahusiano mazuri na jamii inayotuzunguka maana wao ni msaada wa kwanza kwako kuliko ndugu zako walio mbali.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection