Tusilaumu Wala Tusihukumu Wengine

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Lawama ni kitendo cha kumlaumu mtu kutokana na makosa aliyokufanyia kwa kukusudia au bila sababu. Watu wengi hawapendi kufuatilia mambo kwa kina ili kupata ukweli ambapo humfanya mtu aamini mambo bila kuchunguza. Hali hiyo husababisha wengine kuumia ndani kwa ndani bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Aidha, kuna watu ambao ukiangalia kwa juu juu unaweza kuona kuwa wamekosea sana, lakini ukiwasikiliza kwa makini, utagundua kuwa, halikuwa kosa lao. Walaumiwa wengine walijitahidi wasikosee ila walishindwa. Wengine bado walibakia wakijuta na kuendelea kuugua moyoni huku wakilia wakiwa hawafurahii makosa yao.

Pia, wengine waliingizwa kwenye mitego bila kutegemea, hatimaye wakajikuta wamekosea huku wakiendelea kulaumiwa. Hali hiyo pia inawaongezea maumivu, majuto na hata msongo wa mawazo.

Wakati mwingine, wewe mwenyewe unajua kabisa una makosa ambayo unatamani usingeyafanya. Huenda unayajutia na usingependa watu wakukumbushe yaliyopita. Hapo wahukumu wanakuwa ni wengi ila watia moyo ni wachache.

Tunajifunza kuwa, tusiwe watu wa kulaumu tu bila kujua chanzo chake. Yatupasa kama binadamu, 

tuwatie moyo wenzetu waliokata tamaa. Ni jukumu letu kuwafariji ili wasifikie hatua ya kupata msongo wa mawazo na hatimaye sonona ambayo inaweza ikawapelekea hata kwenye kujiua.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Fimbo ya Mbali Haiui Nyoka

Next
Next

Paka Akikuambia Akulindie Samaki Wako, Usikubali