Paka Akikuambia Akulindie Samaki Wako, Usikubali

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Paka ni kiumbe aina ya mnyama anayefugwa. Mara nyingi hupendelea sana kukaa jikoni.

Katika maisha unaweza kupata marafiki mbalimbali. Wengine waaminifu na wengine ambao si waaminifu hata kidogo. Baadhi wanaweza kuja kwako wakiomba mshirikiane kwenye biashara au masuala mbalimbali yahusuyo fedha. Kuwa makini kabla hujaingia naye kwenye makubaliano na kumkabidhi mradi wako ili akusaidie kuuendesha. Jaribu kumchunguza kwanza, usiwe na haraka.

Unaweza ukajikuta umefilisika kwa sababu rafiki yako anaweza akawa na tamaa au akakosa uaminifu kwenye pesa. Utakapogundua hilo, tayari utakuwa umeumia au umeishalizwa.

Tunawaasa vijana, awe msichana au mvulana, nyote mzingatie. Usimuamini rafiki yako kwa kumkabidhi vitu vya thamani ili akulindie. Kabla hujaamua kuingia kwenye mtego huo, fanya uchunguzi wa kina ili ujiridhishe kwanza kama uamuzi wako ni sahihi ama laa. Watu wengi wamelizwa na marafiki waliokuwa wakiwaona kuwa ni marafiki wa kweli na waaminifu. Matokeo yake yalikuwa ni kinyume na walivyotegemea. Kwa hakika, binadamu ni kiumbe wa ajabu, hatabiriki, anaweza akafanya chochote wakati wowote. Hivyo, yatupasa kuwa waangalifu katika mahusiano yetu nao.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Tusilaumu Wala Tusihukumu Wengine

Next
Next

Mwenda Pole Hajikwai