Mwenda Pole Hajikwai

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde. Mara nyingi kupanda mlima huwa kuna ugumu wake na kunahitaji umakini sana ili usikwame njiani ukashindwa kufika juu kunako lengo lako.
Kipindi hicho huwa ni wakati wa utafutaji. Sote tunajua kuwa utafutaji una milolongo mirefu sana. Wengi hupenda kumuangalia yule aliyefika kileleni wakifikiria kuwa ni rahisi kufikia huko.
Wengine huwa wako tayari hata kufanya lolote ikiwa ni pamoja na uhalifu ili wafikie alipo yule wanayemuona kuwa yuko juu. Matokeo yake, ni kuingia matatani na hata kufungwa. Yote hiyo ni kukosa subira na kutaka mafanikio ya haraka haraka.
Sambamba na usemi huu ni ule usemao haraka haraka haina baraka. Inatupasa kuwa na subira katika maisha yetu maana mambo mazuri hayataki haraka na taratibu ndio mwendo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection