Maisha Ni Milima Ya Kupanda Na Kushuka

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha ya mwanadamu yana utaratibu wake wa kupanda na kushuka. Hata ingekuwaje, hakuna mtu anayeweza kuibukia kileleni bila kwenda kwa hatua. Utaratibu uliopo ni kupanda hatua moja baada ya nyingine ndipo ufike kileleni. 

Safari siyo rahisi ndiyo maana wengi huishia njiani. Unaweza kujikuta unakata tamaa. Wengi hufikiria kuwa kama wakikazana kupanda, mambo yao yatakuwa mazuri. Lakini fikra hizo sio za ukweli kwa sababu baada ya kumaliza kupanda mlima moja utakuta kuna milima mingine inakusubiri. Siyo kwamba ukiweza kupanda mlima mmoja basi mambo yako yamekwisha. Unahitaji kupanda milima mingi zaidi. Hayo ndio maisha yetu sisi wanadamu, hakuna ujanja. 

Hivyo ndivyo maisha yalivyo, ukimaliza kutenda jambo moja ujue baada ya muda litakuja tena jingine la kulishughulikia.  . Mathalani, kunaweza kuwa na changamoto mmoja, wakati unashughulikia kuitatua, zinakuja changamoto nyingine za kuzishughulikia.

Hakuna siku utasema umemaliza kupanda milima hiyo na sasa unakaa kileleni tu. Kila siku kutakuwa na milima mingine ya kupanda

Haya ndiyo maisha ya mwanadamu tangu kuzaliwa mpaka kufa kwake. Maisha ya mwanadamu ni safari ya kupanda milima tu. Ni vema ukafurahia safari hizi na sio kufika kileleni, kwani kila mwisho wa safari ya kilele kuna mlima mwingine.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mwenda Pole Hajikwai

Next
Next

Jipe Muda Wa Kufurahia Yale Uliyobarikiwa