Jipe Muda Wa Kufurahia Yale Uliyobarikiwa

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ni jambo la kawaida kabisa kwa binadamu kupenda kuwa na furaha siku zote za maisha yake. Lakini yatupasa tuelewe kuwa furaha hiyo haipatikani ki urahisi. Inakupasa kuhangaika na kujishugulisha ili uweze kutimiza matakwa yako na ufurahie matunda ya kazi zako. Lakini badala ya kujishughulisha, inafikia wakati tunaangalia fulani kafanya hiki au kile na ndio maana kafanikiwa zaidi. Tunafikiria kuwa mafanikio yake huenda yalipatikana kiurahisi. Hatuchukui muda kuchunguza alikotoka hadi akafikia hapo alipo. Tunafikiri yote aliyonayo aliyapata kiurahisi tu.

Badala ya kufurahia kile kidogo tulichojaliwa, tunaanza kushindana na aliye tutangulia. Lakini siyo rahisi ki hivyo, kamwe hatutaweza kulingana na aliyetutangulia.  

Kila mtu alianza kivyake na kwa muda wake. Shida na mikiki aliyopitia mwenzio ni tofauti na yako, na wala huijui.

Unachotakiwa kufanya ni kufurahia kile kidogo ulichobarikiwa kuwa nacho wakati unaendelea kupambana.Tuache tabia ya kuangalia yule ana nini na kuanza kuoneana wivu kwa kile mwenzio alichobarikiwa kuwa nacho.Tunachotakiwa kufanya ni kutiana moyo na kuomba ushauri pale inapobidi. 

Sote binadamu tunahitajiana. Yatupasa tufurahie mahusiano mazuri na binadamu wenzetu na pia kufurahia kile tulichojaliwa kuliko kuoneana wivu ambao utarudisha nyuma maendeleo yetu na ya wengine.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Maisha Ni Milima Ya Kupanda Na Kushuka

Next
Next

Mtoto Wa Mwenzio Ni Wako