Mtoto Wa Mwenzio Ni Wako

Simulizi
by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mtoto ni mwanadamu mwenye umri mdogo ambaye hajafikia kuwa mtu mzima. Kutokana na umri wa mtoto huyu kuwa mdogo, anapaswa apewe malezi bora kama vile, chakula, malazi, malezi, elimu na haki zake zote za kimsingi.
Kwa bahati mbaya, baadhi ya watoto hukosa fursa ya kupata malezi bora. Kwa mfano akina mama wa kambo wengine wana tabia ya kutokuwa na upendo kwa mtoto wa mume aliyemzaa kabla ya ndoa. Hali hii humjengea mtoto chuki, upweke na kumfanya asiwe na raha. Maisha yake huwa ya wasiwasi, akili yake husongwa na mawazo mengi. Hali hii humpelekea kupata hata sonona.
Tunapobagua watoto kwa vile tu hujawazaa wewe bali ni wa mume wako, yatupasa tukumbuke kuwa watoto waliozaliwa na baba au mama mmoja hawatakiwi kutenganishwa kwani wana damu moja inayopita kwenye mishipa yao.
Kuna matukio mengi yanayoambatana na ukatili unaofanywa na baadhi ya mama wa kambo. Taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zikiwemo radio, televisheni na magazeti vinatuhabarisha matukio hayo kila kunapokucha. Watoto wanapokosa mapenzi na malezi hutetereka kimaisha kutokana na msongo wa mawazo na hupoteza mwelekeo.
Hapa tunajifunza kuwa inatupasa kuwa na ubinadamu. Mtoto wa mwenzio ni sawa na mtoto wako. Ni vema, kuwa wakarimu kwao. Tuna wajibu wa kuwapenda kama vile tunavyowapenda watoto tuliowazaa. Tunatakiwa kuwa karibu nao, tuwahudumie sawa na watoto wetu. Hatutakiwi asilani kuwabagua wala kuonyesha tofauti kati yao na watoto tuliowazaa. Tuache roho za ubinafsi, roho za ubaguzi. Sisi sote ni binadamu na isitoshe, safari yetu hapa duniani ni fupi sana. Inatupasa kuwekeza mema ili tuje tuvune mema.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection