Mafanikio Ya Mtu Hutegemea Uwezo Wa Kufikiri Na Kutafakari

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mafanikio ya mtu yeyote hapa duniani hutokana na bidii, kujiamini, kiwango na uwezo wake wa kufikiri na kutafakari. Aidha, wengine hupoteza muda wao kuwaza jinsi watu wengine wanavyowaona, wanavyowafikiria, wanavyowatafakari na wanayowawazia.
Hata hivyo inabidi kujua kwamba, ili uweze kufanikiwa katika maisha, kamwe usitumie muda wako kuwaza kuwa nikifanya hivi wengine watanionaje ama watanifikiriaje. Inakubidi wewe ufanye shughuli zako kwa kujiamini. Ili mradi unachofanya kiwe ni sahihi mbele ya Mungu na mbele za binadamu wenzio.
Kwa kuwa na mtizamo huo chanya, mawazo ya watu wengine hayataruhusiwa kuitawala akili yako. Mtazamo chanya utakufanya usimame imara kwenye kile unachokiamini na hatimaye, utapata mafanikio.
Hapa tunapata funzo kuwa, kamwe tusiumize vichwa vyetu na kuchukua muda mwingi kuwafikiria watu wengine wanachowaza juu yetu. Jiulize wewe unawaza nini kuhusu wao pamoja na kwamba hata wewe siyo kazi yako kuwawazia wengine. Wewe jali kazi na maisha yako na mambo yanayokuhusu. Acha kuwafikiria wao kwani mambo yao wewe hayakuhusu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection