Asiye Uliza Hana Cha Kujifunza

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuuliza ni tendo la kutaka kufahamu au kujua jambo ambalo hulijui au hulifahamu. Inawezekana pia hilo jambo unalifahamu lakini huna hakika kama hicho unachokifahamu ni sahihi. Kwa hiyo unatafuta kuelekezwa zaidi na mtu mwingine.
Kwa jinsi hii unataka kujifunza zaidi ili upate ufahamu zaidi. Kwa mfano, mwanafunzi anayeuliza maswali mara nyingi ndiye ambaye huwa anafaulu na kuelewa zaidi kuliko asiyeuliza. Anayeuliza, anapata majibu ya yale ambayo hayajui ama si mzoefu nayo.
Katika maisha, hakuna mtu ambaye anazaliwa akiwa anajua kila kitu. Sote tunajifunza kwa kuona na kusoma. Usemi huu unatufundisha tusiwe watu wa kuridhika na kile tulichojaliwa nacho. Tuendelee kupambana na tusiogope kujifunza zaidi na zaidi. Maana maisha ni mapambano na elimu haina mwisho. Hali kadhalika, wahenga walisema, ‘Kuuliza si Ujinga’, hivyo tutumie fursa tunazozipata kuuliza mambo tusiyoyaelewa. Kumbuka, binadamu tunategemeana kwa mambo mengi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection