Siyo Kila Unalofanya Litampendeza Mwingine

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika jamii inayotuzunguka siyo kila mtu ni mzuri kwako, laa hasha. Wabaya wapo wengi pia. Kuna watu ambao hawapendi mafanikio au maendeleo ya watu wengine. Mara nyingine unajikuta kwenye jamii ambayo kila wakati unapingwa na kudharauliwa. Kila utakachofanya unakosolewa bila sababu ya msingi. Binadamu kwa kweli ni kiumbe wa ajabu.

 Hebu tuangalie mfano halisi kwenye uwanja wa mpira. Watazamaji waliopo nje ya uwanja huona mchezo wa mpira kuwa ni mwepesi na kwamba hauhitaji ufundi wowote. Huwaona wale wanaocheza kuwa ni wazito na hawachezi vizuri. Wengi hufikia hata hatua ya kushangaa kwa nini hawafungi magoli. Hujigamba na kusema kuwa wangelipata wao fursa ya kucheza mpira, wangeweza kucheza vizuri zaidi kuliko hao. Ukweli ni kwamba, walioko nje ya uwanja hawana ubavu wa kuwakosoa wachezaji kwa sababu wao ni watazamaji tu. 

Hata hivyo, kuna wanadamu wengine ambao ni mafundi na wana tabia ya kuwakosoa wenzao hata kama hakuna sababu. Sasa basi hebu jaribu kuwapa nafasi kama hiyo uone kama wataweza kufanya vizuri zaidi. Unaweza kuja kushangaa kuona jinsi watakavyoharibu mambo. Wako wale wanaopenda kukosoa kwa sababu tu ya wivu. Aidha wanataka waonekane kuwa wao ndio bora zaidi. Wengine huwa na hulka ya kupenda kufahamika zaidi kwa watu.

Fundisho kubwa tunalopata hapa ni kwamba hapa duniani kamwe huwezi kumpendeza au kumfurahisha kila mtu kwa kila ufanyacho. Cha msingi, unatakiwa ujitambue. Yakupasa ujue unahitaji kufanya nini na kwa faida ya nani. Usikate tamaa, jitahidi kadri unavyoweza kupambana na maisha bila kushinikizwa na mtu yeyote. Usisikilize maneno ya pembeni kwani ni vitisho vya kukutia hofu tu kutoka kwa wabaya wako. Kuwa imara na mwenye mwelekeo kwenye maisha yako. Usisumbuke na binadamu kwani hawatosheki.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Asiye Uliza Hana Cha Kujifunza

Next
Next

Zimwi Likujualo, Halikuli Likakwisha