Zimwi Likujualo, Halikuli Likakwisha

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha, watu tunaishi kwa kufahamiana na kujuana. Kuelewana huko kuko katika tabaka mbalimbali, mathalani, kwenye jamii zetu, familia zetu na hata kwenye makundi maalumu. Hata kwenye sehemu za kazi matabaka haya ama makundi haya hujitokeza sana. Huwa kuna upendeleo dhahiri unaotokana na kufahamiana, hilali hiyo ipo.

Mambo haya hata kwenye uongozi yapo. Kiongozi huwa anapenda kuwatambua jamaa zake pamoja na ndugu zake ili aweze kuwaweka na kuwapanga kwenye nafasi nzuri mbalimbali. Mara nyingine wateule wake hao, huwa hawana hata uwezo au uwezo wao mdogo. Lakini pamoja na hayo, upendeleo wake bado utabaki pale pale.

Hali hiyo ya upendeleo tunaiona katika sehemu na ngazi mbalimbali. Upendeleo ndio unaotembea mara nyingi. Sambamba na huo usemi ni ule usemao mbiu huanzia nyumbani. Huwezi kumpelekea jirani chakula wakati watoto wako hawajala. Ni ubinadamu kujali kwanza mambo yanayokuhusu na ndipo uyaangalie. ya wengine. Mambo yote mengine huja baadaye. Hapo tunaweza kusema, binadamu ni wabinafsi, ndivyo tulivyoumbwa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Siyo Kila Unalofanya Litampendeza Mwingine

Next
Next

Debe Tupu Haliachi Kutika