Debe Tupu Haliachi Kutika

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tupo katika ulimwengu wenye mambo mengi yanayotuzuguka. Kwa kawaida, maisha yetu yako katika makundi makundi. Yapo makundi yenye uwezo mkubwa, yapo yale yenye uwezo wa kati, hali kadhalika yale ya kawaida. Kundi hili la mwisho ni lile ambalo inawezekana hata riziki ya siku ni ya kubabaisha. Inaweza hata siku ikapita bila ya kuwa na chochote.
Katika hayo makundi kuna kundi ambalo huwa linapenda kuongea sana na kujinadi kuwa lina uwezo wa kufanya hili au lile. Yote hii ni katika kutaka kujilinganisha na kundi lingine. Mara nyingi, kundi hilo huwa ni lile kundi la chini. Wao hupenda kulingana na wale wa matawi ya juu. Huwa wana porojo nyingi na kujitamba sana.
Pamoja na kwamba hata hayo makundi mengine hayakosekani kuwa na watu wa aina hiyo, lakini ni kwa uchache. Wengi wao huwa wanaonekana kwa matendo yao na maisha yao ya siku hadi siku. Lakini kwenye usemi huu wa Debe Tupu Haliachi Kutika,kundi la chini ndilo linalolengwa. Sambamba na usemi huu, upo ule usemao ‘Pakacha Halikingi Maj’. Hapa na sisi tunashauriwa kuwa majigambo hayafai, bali tuonyeshe tunachokifanya machoni pa watu kwa vitendo. Maneno peke yake hayafai kabisa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection