Kumbuka Kuna Kesho

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Unapoishi na watu hapa duniani, tambua kuwa kuna kesho. Aidha, unapokuwa kiongozi wa watu sehemu fulani kumbuka pia kuna kesho. Unapokuwa na madaraka, nafasi ya juu, kipato kizuri, na mwenye kutoa maamuzi ya juu, kumbuka kuna kesho. 

Ukimuona leo mtu hakufai, eti kwa sababu tu hana chochote, hana mwelekeo, na hana mvuto, pia ni wa hali ya chini, na siyo wa aina yako, kesho unaweza kumhitaji na akakufaa kuliko ulivyotegemea.

Kwa mfano, yule unayemwona kwa sasa hakufai, hujui kesho yake, anaweza kukufaa siku nyigine kwani hakuna mtu ambaye ni maskini na akakosa kitu cha kutoa au kumsaidia mwingine. Kila mtu ana thamani kwake mwenyewe na kwa watu wengine. Hivyo kama wewe unajiona ni tajiri ambaye unajitosheleza, unajiona kuwa huhitaji msaada wowote ule, ni vema ukatambua kuwa bado hujajitosheleza bila kuwategemea wenzio. Ni sawa unajiona umejitosheleza, lakini ipo siku utawahitaji hao unaowaona huwahitaji leo kwani hakuna binadamu aliyekamilika. Wasaidie wenzio kile wanachohitaji bila kinyongo chochote na wao watakusaidia kwa mambo mengine. 

Maisha ya mtu ni fumbo kubwa sana pia ni mzunguko, leo mimi, kesho wewe, kila mtu ana umuhimu katika maisha ya mwenziwe.

Kama binadamu hatutakiwi kudharauliana. Yatupasa wote tuheshimiane bila kubaguana kutokana na maumbile, kipato, kabila au dini. Binadamu sote tuko sawa na tuko safari moja ambayo ni fupi sana. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Debe Tupu Haliachi Kutika

Next
Next

Kua Makini, Chunguza Ushauri Unaopewa Kabla Ya Maamuzi