Usisamehe Kama Hauko Tayari Kusahau

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Msamaha ni jambo la kiungwana ambalo mtu anafanya au anatakiwa kufanya kwa mtu ambaye amemkosea au kumuudhi katika jambo lolote. Kwa watu wengi, kuomba msamaha huwa siyo jambo rahisi, huwa kuna ugumu fulani. Ugumu huu hutokana na ile tabia ya kushindana na kujihesabia haki. 

Neno msamaha ni neno dogo sana lakini kulitamka ama kumtamkia mtu, hata kama unaelewa kuwa umemkosea huwa inakuwa ngumu na tabu kwa kiasi fulani. Mara nyingine unaweza ukasamehe kwa kutamka tu bila dhamira kutoka moyoni. Lugha iliyotumika katika utoaji wa msamaha huo inaweza ikaonyesha dhahiri kuwa msamaha huo ni wa kinafiki. 

Hapa nataka kusema kuwa kuna wengine wanatoa msamaha lakini pale anapokutana na mtu mwingine anaanza kuongelea jambo lile lile ambalo alikuwa amelitolea msamaha. Inapotokea hivyo ndipo inaposemekana kuwa msamaha wako ulikuwa ni wa kinafiki na hapo ndio inakuwa hujasamehe. 

Jambo ulilolitolea msamaha unatakiwa usilikumbuke tena. Unaposema sitasahau, yule alinifanyia vile lakini nimemsamehe, hapo ukweli ni kwamba unakuwa bado hujamsamehe kwa dhati. 

Maandiko yanasema kuwa tusamehe ili naye Muumba aweze kutusamehe. Sote tunajua kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu. Ni bora usisamehe kabisa kama bado unatunza kumbukumbu ya kukosewa. Hapo inaonyesha dhahiri kuwa kutokuwa tayari kusahau ni sawa kabisa na kusema bado hujasamehe. Vitendo vyako ndiyo ishara kubwa ya kuonyesha hivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Chui Hakumbatiwi

Next
Next

Umdhaniaye Siye