Kujifunza Ni Kila Siku

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kama unatamani kuwa vile unataka kuwa, jitahidi uvuke kawaida ya mfumo unaozaa wale wanaokuvutia.
Kama unataka kuwa mtu uliyefanikiwa zaidi ya wale unaowaona wamefanikiwa, jitahidi mno uvuke kawaida, ili uende zaidi ya pale walipoishia.

Na kama unataka kuthibitika kwenye eneo unalohitaji kufanikiwa, hakikisha unaendelea kujifunza kuishi inavyopaswa kwenye hilo eneo. Usipofanya hivyo, kuna siku mtu mwingine atakuja kulitwaa taji yako.

Tatizo kubwa kuliko yote ni kuacha kujifunza na kudhani unacho cha kufundisha wengine wakati bado unahitaji kujifunza kila hatua unayoifikia.

Tunatakiwa kuelewa kuwa kila siku kunatokea mabadiliko na maboresho katika maeneo mbali mbali. Kwa hiyo kujifunza hakuna mwisho, ni jambo endelevu. Kazi ya kujifunza itaisha pale utakapoondoka kwenye hii dunia.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mkono Ukupigao Ndio Ukufunzao

Next
Next

Heri Kuaminiwa Kuliko Kupendwa