Heri Kuaminiwa Kuliko Kupendwa

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Siku zote, binadamu huwa tunataka kupendwa, na si vinginevyo. Huo ni ubinadamu kabisa, hakuna cha ajabu hapo. Mtu anakuwa na furaha pale anapogundua kuwa watu wanamfurahia na kumpa sifa nyingi za kumfanya aonekane ni mtu muhimu katika jamii. Lakini ni lazima tukumbuke kuwa inawezekana hao wanaokumwagia sifa wana sababu zao. Pengine ni unafiki tu na huenda kuna jambo wanalolitaka kutoka kwako. Furaha yako isiwe ya kukurupuka tu, yakupasa utafakari kwanza. Huenda mtu huyo ana jambo ambalo anataka asaidiwe katika eneo fulani linalomsumbua. Anajua kuwa ataweza kusaidiwa pale atakapokumwagia sifa lukuki.
Pamoja na kwamba huwa tunaaswa kuwa tupendane, inatubidi tuangalie mazingira ya kupendana kwenyewe.
Mara nyingi imetokea kuwa wapendanao ndio wakosanao.
Kulitokea vijana wawili ambao walikuwa marafiki na mambo mengi walikuwa wakiambizana. Moja kati yao alimuazima mwenzie kiasi kikubwa tu cha fedha. Mkopaji aliahidi kuwa atamrudishia baada ya muda mfupi. Lakini kutokana na matatizo ya hapa na pale hakufanikiwa kurudisha kwa muda alioahidi. Hapo ndipo uhasama ulipoanzia. Jamaa aliingia mitini, imani ikawa imemtoka hadi wakafikishana mahakamani. Kuaminiana kite kuliisha na ukaribu wao ulikufa. Inaonekana jamaa alifikiri kuwa akimweleza atamuamini, lakini haikuwa hivyo.
Usemi huu unatufundisha kuwa tukiazima kitu cha mtu tuwe makini kukirudisha kwa wakati tulioahidi. Hapo tutajenga ile hali ya kuaminiwa, na kila mtu atakusifu kwa uaminifu wako. Ndio maana watu wanasema, bora kuaminiwa kuliko kupendwa. Kuaminiwa ni kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection