Hakuna Anayefika Juu Kwa Kulala Usingizi

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Yatupasa tujue kuwa tukipenda usingizi hatutafika popote kimaendeleo. Hiyo huwa ni dalili tosha ya kuukaribisha umaskini. Tumeshuhudia wenyewe katika maisha yetu ya kila siku. Watu wengi wenye juhudi ya kufanya kazi kwa bidii wana maisha mazuri. Wana uwezo wa kusomesha watoto wao, uwezo wa kula vizuri, hali kadhalika, uwezo wa kuwa na nyumba nzuri za kuishi.

Ukiwachunguza watu wa namna hiyo, utagundua siri fulani. Watu hawa huwa wanachelewa kulala. Na siyo hivyo tu, huamka mapema sana na kwenda sehemu ya kujipatia kipato. Kwa kufanya hivyo, yaani kujibidisha, ndipo mtu ataweza kufikia malengo aliyojiwekea.

Inafurahisha kuona watu wengi sasa hivi wamelitambua hilo. Watu wamekuwa wakipambana kwa staili mbalimbali ili familia zao ziweze kumudu maisha kwa kupata vile ambavyo vinahitajika katika maisha yao ya kila siku.

Kutokana msemo huu, tunajifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii. Hatutakiwi kuendekeza usingizi kwani hauna faida katika maisha. Wengi waliouendekeza usingizi, waliishia kuwa maskini, tena maskini wa kutupa.

Mara nyingi, uvivu huleta hata mifarakano ndani ya familia. Inafika wakati ukiomba msaada kutoka kwa na ndugu wanaweza wakakataa kukusaidia. Pale utakaponyimwa msaada, utajiona kuwa ndugu au jamaa zako hawakupendi. Ukweli ni kwamba uvivu wako ndio unaosababisha hayo. Suluhisho la yote ni kuacha uvivu. Hali kadhalika, unatakiwa kuwa na uthubutu. Yakupasa uendeshe maisha yako mwenyewe na siyo kutegemea watu wengine. Usemi wa ‘Mtumai cha ndugu, hufa maskini’, unadhihirisha uhalisia huu. Kila mtu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii. Hata maandishi matakatifu yanasema, ‘Asiyefanya kazi na asile.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Heri Kuaminiwa Kuliko Kupendwa

Next
Next

Hatuwezi Kuibadilisha Jamii Kama Hatujabadilisha Familia Kwanza