Hatuwezi Kuibadilisha Jamii Kama Hatujabadilisha Familia Kwanza

Margaret Kayombo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Jamii inajumuishwa na mkusanyiko wa familia mbalimbali zinazoishi kwa pamoja kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za nchi. Katika hali ya kawaida tunategemea kuwa na jamii ambayo ina maadili mema ya kuweza kuliletea sifa njema Taifa letu.

Ukweli ni kwamba, kwa sasa mambo sivyo yalivyo. Hali imekuwa kinyume na tofauti na matarajio yetu. Ni kilio kila sehemu katika jamii yetu kutokana na kumomonyoka kwa maadili. Kundi kubwa la vijana wetu wamekuwa visivyo. Wamekuwa kama vile hawana wazazi wa kuwaongoza au kuwaelimisha jinsi ya kuishi kiustarabu.

Kutokana na hali hiyo, inatupasa tujiulize swali la msingi, ‘Je tutaendelea kuwa na kizazi cha aina hiyo mpaka lini’? Pengine jibu la swali hilo linaweza kuelekezwa kwetu sote, nalo ni:“ Sote tuanze kubadilisha familia kwanza na ndipo tutegemee jamii yote ya Tanzania ibadilike na hivyo kuwa na maadili mema na taifa lenye sifa njema duniani.

Je, tutabadilishaje familia zetu? Wazazi, ambao ni baba na mama kuzingatia wajibu wao wa kulea watoto. Yawapasa wawapatie watoto wao malezi yenye misingi bora ya kuishi ili waweze kukabiliana na majaribu yoyote katika maisha yao.

Wazazi wengi sasa hivi hawana muda huo. Muda wao mwingi wanautumia katika kutafuta pesa na mambo mengine. Kwa walio wengi, malezi ya watoto wao siyo ya muhimu. Tunaweza tukasema, watoto wanafugwa siku hizi kuliko kulelewa. Mara nyingi wazazi wanachukua hatua ya kuwa makini na malezi ya watoto wao wakiwa tayari wamekwisha haribika. Ni sawa sawa na kufunga zizi, wakati ng’ombe wote wamekwisha toka! Hapo itakuwa haisaidii kwani zizi ni tupu. Kwa maana hiyo inakuwa ngumu kuwaweka watoto kwenye misingi bora wakati huo kwani unakuwa umechelewa. Ni kama ule usemi unaosema “Samaki Mkunje Angali Mbichi”.

Kutokana na usemi huu, wazazi tunaaswa tubadilike na pia tuwajibike katika malezi ya watoto wetu. Tusiwafuge, watoto ni binadamu. Hali kadhalika, wazazi tunatakiwa tuwe na kiasi katika shughuli zingine za kutafuta pesa na mambo mengine. Kipaumbele kiwe ni kwa watoto. Hali kadhalika, tuache kuwalaumu watoto, tusiwanyoshee vidole wakati makosa ni yetu sisi wazazi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hakuna Anayefika Juu Kwa Kulala Usingizi

Next
Next

Ndoa Ina Furaha, Na Maumivu Pia